Thursday, May 21, 2015

Siyo Njia Yangu, Bali Ya Mungu

Siyo Njia Yangu, Bali Ya Mungu
Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Zaburi 25:4,5.
Maelekezo yaliyotolewa kwa Musa yalikuwa, "Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima" (Waebrania 8:5). Ingawa Musa alikuwa amejawa na ari ya kufanya kazi ya Mungu na angeweza kuwa na watu stadi zaidi, walio na talanta ya kutekeleza mapendekezo yoyote ambayo angewapa, ilimpasa asitengeneze hata kitu kimoja, iwe kengele, komamanga, tarazo, kishada, pazia au chombo chohcote isipokuwa kulingana na mfumo uliooneshwa kutokana na wazo kamili al Mungu. Kwa siku arobaini alipewa ujumbe na aliposhuka hadi chini ya mlima alikuwa tayari kueleza mfumo halisi kama alivyooneshwa mlimani.
Pale ambapo wengi wamekosea, hawakuwa waangalifu katika kufuata mipango ya Mungu, bali iliyo yao. Kristo mwenyewe alisema, "Mwana ahwezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda" (Yohana 5:19). Alijivua nafsi yake kikamilifu kiasi ambacho hakufanya mipango na taratibu zake. Kama Yesu alimtegemea Mungu kikamilifu hicyo na kusema, "Chochote nimwonacho Baba akikifanya ndicho ninachokifanya," mawakala wa kibinadamu wanahitaji zaidi kumtegemea Mungu kwa maelekezo ya kudumu, kwa namna ambayo maisha yao yatakuwa eneo la zoezi kwa ajili ya mipango ya Mungu!
Njia zetu wenyewe zinaweza kushindwa. Kiburi, kujipenda nafsi, sharti visulubiwe na ombwe linalosalia lijazwe na Roho na nguvu ya Mungu. Je, Yesu Kristo, Mfalme wa mbinguni, amepewa nafasi? Umemtazama, roho yake ilipotabika Gethsemane, akiomba kwa Baba yake? Ni kiut gani kilichoweka msukumo kiasi cha matone ya damu kutokana na maumivu kwenye kipaji chake kitakatifu? Ah, dhambi za dunia yote zilikuwa juu yake! Kutengana na upendo wa Baba yake ndiko kulikolazimisha kauli hii itoke kwenye midomo iliyopauka na kutetemeka, "Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke" (Mathayo 26:39). Aliomba hivi mara tatu, lakini baada yake akasema hivi "Walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke" (LUka 22:42). Sharti huu uwe ndio mtazamo wetu - isiwe mapenzi yangu, bali yako, Ee Mungu yatimizwe. Huu ndio uongofu wa kweli.

No comments:

Post a Comment