Thursday, May 21, 2015

Uhuru Kwa Njia ya Kristo

Uhuru Kwa Njia ya Kristo
Katika uungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Wagalatia 5:1.
Hapo mwanzo Mungu alimweka mwanadamu chini ya sheria kama sharti muhimu sana kwa ajili ya maisha yake. Alikuwa chini ya serikali ya mbinguni na haiwezekani kuwa na serikali bila kuwa na sheria...
Mungu ni mwenye uwezo wote, mwenye ujuzi wote, asiyekosea. Daima anatafuta mwelekeo ulionyooka. Sheria yake ni ukweli usio na kosa, ukweli wa milele. Kanuni zake zinapelekana na tabia yake. Lakini Shetani anazifanya zionekane katika nuru isisyo ya kweli. Kwa kuzipotosha, anatafuta njia ya kuwapa wanadamu picha isiyofaa ya yule Mtoa sheria. Katika uasi wake wote ametafuta kuwmakilisha Mungu kama Mungu asiye haki na dhalimu.
Kutokana na kutokutii kwa Adamu, kila mwanadamu ni mvunjaji wa sheria, akiwa amewekwa chini ya sheria. Asipotubu na kuongoka, anakuwa chini ya utumwa wa sheria, akimtumikia Shetani, akiangukia kwenye udanganyifu wa adui na akisema kinyume na kanuni za Yehova. Lakini kwa kutii kikamilifu matakwa ya sheria, mwanadamu anahesabiwa haki. Utii huo unawezekana kwa njia moja tu ya imani katika Kristo. Watu wanaweza kuelewa upande wa kiroho wa sheria, wanaweza kutambua uwezo wake kama kigunduzi cha dhambi, lakini hawawezi kuukabili uwezo wa Shetani na udanganyifu wake, kama wasipokubali upatanisho ambao wamepewa kupitia kwenye kafara ya Krsto inayoponya, ambaye pia ni Upatanisho wetu - "Kipatanishi" chetu na Mungu.
Wale wanaomwamini Kristo na kutii amri zake hawapo katika utumwa wa sheria ya Mungu; kwani kwa wale wanaoamini na kutii, sheria yake sio sheria ya utumwa, bali ya uhuru. Kila amwaminiye Kristo, kila anayetegemea uwezo unaotunza wa Mwokozi aliyefufuka aliyeteseka kutokana na adhabu iliyotolewa kwa mvunja sheria, kila anayepinga majaribu akiwa katikati ya uovu na kuiga mfano unaopatikana katika maisha ya Kristo, atakuwa mshirika wa tabia ya Mungu kwa njia ya imani, akiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. Kila mtu ambaye kwa imani anatii amri za Mungu atafikia hali ya kutokuwa na dhambi ambayo Adamu alikuwa nayo kabla ya kuvunja sheria.

No comments:

Post a Comment