Tuesday, June 30, 2015

UZURI WA TABIA YA KRISTO

UZURI WA TABIA YA KRISTO
Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. Mithali 22:1.
Watu wanaweza kutamani umashuhuri. Wanaweza kutamani kuwa na jina kubwa. Baadhi hutamani kumiliki nyumba, mashamba, na wingi wa fedha, kile kiwafanyacho wawe wakuu kulingana na viwango vya kidunia, ndicho kilele cha shauku yao. Wanatamani kufikia mahali pa juu kimafanikio ambapo wanaweza kuwaangalia wengine wote walio maskini kwa chini. Wote hao hujenga mchangani, na nyumba zao zitaanguka ghafla. Ukuu wa kimadaraka siyo ukuu halisi. Kile kisichoongeza thamani ya roho hakina thamani yoyote kwa chenyewe. Kitu cha thamani kuu ni kupokea ukuu halisi wa roho machoni pa Mungu. Unaweza usijue ukweli na hadhi ya kazi yako. Unaweza kupima tu thamani ya uhai wako kwa kulinganisha na thamani kuu ya Mwokozi aliyeutoa uhai wake kuwaokoa wote watakaompokea.
Kila mtu anaweza kupata makadirio ya thamani ya roho yake pale anapokubali kuwa mtendakazi pamoja na Kristo, akitenda kazi aliyoitenda Kristo, kuijaza dunia kwa haki ya Kristo,, akitii agizo la utume la Aliye Juu. Agizo hilo la injili walilopewa wanafunzi wanapatiwa wale wote waliounganishwa na Kristo. Inawapasa kujikana nafsi kwa kila hali ili kupata furaha ya kuziona roho zinaokolewa ambazo bila Yesu zingalipotea.
Heshima kuu wanayoweza kupewa wanadamu, vijana kwa wazee, matajiri kwa maskini, ni kule kushirikishwa katika kuwaweka huru wanaoonewa na kuwafariji wanyonge. Dunia imejaa mateso. Nenda, ihubiri injili kwa maskini, waponye wagonjwa. Hii ndiyo kazi ya kuunganishwa na ujumbe wa injili. "Maskini wanahubiriwa habari njema" (Mathayo 11:5). Watendakazi pamoja na Mungu inawapasa kujaza nafasi wanayoimiliki katika ulimwengu huu kwa upendo wa Yesu. Upendo wa Kristo moyoni hudhihirishwa kivitendo. Iwapo upendo wa Kristo ni baridi, upendo kwa wale ambao Kristo aliwafia utapoa.
Utajiri wa kweli ni imani thabiti na upendo wa kweli. Sifa hizi hufanya tabia ikamilike katika Kristo. Iwapo ingalikuwepo imani zaidi iliyo sahili yenye kumtumainia Yesu, kungalikuwepo upendo, upendo wa kweli, ambao ndio dhahabu ya tabia ya Kikristo.

No comments:

Post a Comment