Tuesday, June 30, 2015

MTANDAO WA MIVUTO YA WEMA

MTANDAO WA MIVUTO YA WEMA
Mimi ni rafiki ya wote wakuchao, rafiki yao wanaozitii kanuni zako. Zaburi 119:63.
Vijana wanapenda kupata marafiki kulingana na kiasi cha hisia zao na mapenzi yao wanapofungamana na wale wanaoshirikiana nao, na ndivyo mvuto wa rafiki hao utakavyokuwa na nguvu zaidi juu ya vijana hao, iwe ni kwa baraka au kwa laana. Hebu wazazi wajihadhari. Hebu wachunge kila mvuto wa uhusiano na wengine. "Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia" (Mithali 13:20). Vijana watakuwa na marafiki nao wataathiriwa na mvuto wao.
Kama vile lakiri isivyoweza kukwepa kudumisha sura ya muhuri ndivyo ambavyo akili haiwezi kukwepa kudumisha mivuto iliyosababishwa na maingiliano na kuhusiana na wengine. Mvuto huo huwa kimya kimya usio dhahiri, hata hivyo ni wenye nguvu na mguso mkuu. Iwapo watu wema wenye hekima ndiyo wamewachagua wawe marafiki, basi umejiweka kwenye mazingira mazuri ya kuwa safi kiakili, kimawazo na mwenye mwenendo adilifu. Na ushirika wa jinsi hiyo ni wa thamani kuu katika uundaji wa tabia. Mtandao wa mivuto ya wema itakuzunguka, ambayo yule mwovu hawezi kuivunja kupitia hila zake za udanganyifu.
Hebu vijana watambue kuwa endapo watajihusisha na mivuto na watu wenye tabia na mwenendo mbaya, watachafuliwa. Taratibu lakini kwa hakika mivuto hiyo isiyofaa itaathiri maisha yao na kuwa sehemu ya mwenendo wao, hivyo kuwafanya watembee ukingoni mwa jabali bila kutambua hatari inayowakabili. Wanajifunza kupenda maneno yatokayo katika ndimi laini, maneno yaliyokolezwa asali ya yule mdanganyifu mkuu, nao hawatulii, hawapati amani, hawafurahii hadi pale wapelekwapo kwenye mnara wa ulaghai mkuu wa mtu fulani. Kutembea katika shauri la wasio haki ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kusimama katika njia ya wakosaji na kuketi barazani pa wenye mizaha.
Usalama pekee kwa kijana ni kuchanganyika na wale wenye maadili safi na mwenendo mtakatifu, hivyo mwelekeo mwovu wa utendaji dhambi unadhibitiwa. Kwa kuchagua marafiki wenye kumcha Bwana, watajenga ujasiri wa kiimani isiwe rahisi kwao kutoliamini neno la Mungu, au kupendelea tabia ya mashaka na ukafiri. Nguvu ya kielelezo hai ni muhimu kwa mvuto wa wema.

No comments:

Post a Comment